Friday, 21 March 2014

USALA WA TAIFA KUIBUA HOFU KWENYE VYOMBO VYA HABARI KESHO

Mpango kabambe ulio sukwa na UWT kwa kuyatumia magazeti matatu kesho  umesukwa na frontpage za magazeti hayo kesho zitakuwa na habari mbili kuu.

1. Hotuba ya Jk
2. Hotuba ya Warioba.

1. Hotuba ya jk

Hii imeundiwa zengwe kuwa ndio itakuwa hotuba bora kuliko ya warioba, wabunge wa ccm na wale wa makundi mengine wanaounga mkono ccm  wamepangwa kushangalia sana wakati jk akiwasilisha hasa kuhusu hoja ya serikali 3. Hofu atahengwa kwenye magazeti hayo niliyotaja kuwa nia ya warioba na tume ni kuondoa umoja wa kitaifa uliopo na hatimae kuvunja muungano.

Wazinzibar waishio bara na wale wa bara waishio visiwani wameshajazwa hofu hii kuwa watapoteza kila kitu walicho chuma.

2. Hotuba ya mzee warioba.

Pamoja na kwamba ukweli wa hoja ulionekana kwenye wasilisho la mzee warioba, kesho zitaibua propaganda kuwa hotuba yake haikujali gharama za serikali 3 na tunu ya muungano ambayo kupitia serikali 3 unakwenda kufa. Kumbukeni kuwa kazi ya rais si kwenda kuhutubia bunge kwa kujibu hoja za Warioba bali kulifungua bunge maalumu, chanzo cha uhakika kinasema hatazindua tu bunge lakini atagusa baadhi ya hoja ambazo kimsingi ccm kama chama kinazisimamia kwa nguvu zao zote. Tayari kuna uhakika kuwa sehemu ya hotuba yake imegusa kwa kiasi kikubwa swala la muungano na serikali mbili.

No comments:

Post a Comment