TAASISI ya Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) kwa
kushirikiana na tasisi ya mtandao wa usambazaji wa huduma (IPS network)
imeingia katika soko la pamoja la mawasiliano kwa nchi za Afrika
Mashariki kwa kuzindua mtandao mpya wa simu za mkononi uitwao Smart.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart, Abdellatif Bouziani, alisema
wameamua kuanzisha mtandao huo kwa kutambua changamoto nyingi
zinazoikumba sekta ya mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki na
kwamba mtandao huo utarahisisha mawasiliano na kwa gharama nafuu.
“Mtandao wa ‘Smart Lets Talk’ utawawezesha watumiaji wa hali zote
kumudu gharama za mawasiliano kwa kuwa mteja ataweza kupiga simu kwa
mara ya kwanza hadi atakapokata kwa shilingi 79,” alisema.
Watanzania tunahitaji mawasiliano bora kwa gharama nafuu, siyo utitiri wa mitandao
ReplyDelete