Kinachojiri sasa Bungeni; kwa maandalizi ya
Hotuba ya Rais Kikwete
--------------------------------------------------------------------------------
- Wabunge wanaingia kwa wingi ukumbini.
Naona leo hali ya mahudhurio imekuwa nzuri
- Kwa mujibu wa Ratiba ni kwambq kikao cha
abunge kilipaswa kuanza saa 9.10. Ila ratiba
itachelewa kidogo.mwageni waliofika ni
Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Mkuu wa
Tanzania na Zanzibar
- Mzee Karume naye yupo nje ya viwanja vya
bunge
- Naam namuona Mheshimiwa Freeman
ambowe anawasili na sasa anateta jambo na
ajames Mbatia
- Naam, kule nje namuona Makamu wa Rais,
Gharib Bilal
- Hakika ukumbi wa bunge umependeza sana
leo. Wabunge wengi wamejitokeza na kuna
wageni wengi pia
- Naaam sasa Rais JK anaingia Ukumbini kwa
kupitia ule mlango wa VIP
- Mheshimiwa Abeid Amani Karume sasa
Anaingia
- Mzee Ruksa, Ali Hassan Mwinyi anaingia
sasa
- Jaji Mkuu wa Zanzibar, Jaji Makungu
anaingia Bungeni sasa
- Jaji Mkuu, Mohamed Chande aorhman
anaingia sasa
- Makamu wa Kwanza wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif
Hamad anaingia ukumbini
- Anayefuata ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar, Ali Mohamed Shein
- Anayefuata ni Makamu wa Rais, Dr
Mohamed Ghalib Bilal
- Wageni wote muhimu wamewasili na sasa
anayesubiriwa ni Mheshimiwa Rais kuingia
Bungeni
- Naam mzee wa Speed and Standard
anamsindikiza Rais JK kuingia ukumbini.
Mayowe yanapigwa kuashiria furaha ya
wabunge. Namuona mheshimiwa mnyaa
anapiga meza muda wote
- Mzee Malecela naye yumo. Pia kuna Pius
Msekwa, mama Maria Nyerere na wake za
viongozi
--------------------------------------
- Rais JK anaanza kuhutubia kwa kucheka na
kusema "haijapata kutokea". Sijui ana maana
gani...
- Rais anawaponyeza Mwenyekiti na Makamu
mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwa kishindo.
Anawapongeza pia wabunge kwa fursa hii
waliyopata ya kuwa wabunge wa bunge la
katiba. Anasema kuwa wabunge watatunga
katiba inayokubalika na watanzania,
inayotekelezeka, itakayoondoa changamoto za
muungano zilizopo, itakayoimarisha
muungano, itakayodumisha amani na
usalama, itakayostawisha demokrasia,
kuimarisha utawala wa kisheria, kupunguza
maovu, kukuza uchumi na kuleta maendeleo
sawia kwa wananchi
- Rais anasema kuwa hii ni mara ya Tatu
Tanzania kuandaa katiba. 1965, 1977 na huu
wa sasa. Ila anasema huu wa sasa
unashirikisha wananchi kwa kutoa maoni yao,
mabaraza ya katiba na kwa kura ya maoni.
Tofauti na michakato iliyotanguloa ambapo ni
wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano
tu, mchakato wa sasa una wengi na
unashirikisha makundi mengi
- Rais anasema kuwa kelele za kutaka kuwa
na katiba mpya zimekuwepo sana wakati wa
mfumo wa vyama vingi
- Anampongeza jaji Warioba na wajumbe
wote wa tume.
- Suala la mawaziri kutokuwa wabunge
nalo anataka litafakariwe kwa makini.
Anawataka wajumbe watafakari kwa
kina kuhusu hilo. Kwamba lina uzuri
na ubaya wake
- Sasa anajadili kuhusu muundo wa
Muungano. Anasema kuwa jambo hili
limezua mjadala mzito tangu Rasimu
ya mwanzo hadi ya mwisho. Anasema
kuwa jambo hilo linasubiriwa kwa
hamu na watanzania wengi. Karika hilo
anaroa ushauri ufuatao
1. Wabunge waepuke jazba wakati wa
kujadili suala hilo
2. wajumbe watafakari madhara
yanayoweza kujitokeza iwapo
jambo hilo halitapatiwa ufumbuzi
kwa njia ya utulivu
- Anasema kuwa mjadala wa muundo
wa katiba moya si mheni kama
alivyoeleza Warioba. Kwamba mwaka
1984 ulikuwa chanzo cha machafuko
Zanzibar. Pia mwaka 1993 jambo hilo
lilikuwa ni chanzo na G55
- Rais Kikwete anasema kuwa sababu
za kuwa na serikali mbili ni mbili
1. Kuhakikisha kuwa Zanzibar
haimezwi kwenye Muungano
2. kuepuka gharama kwa Tanzania
Bara kugharamia serikali ya bara
na ya muungano
- Rais anasema kuwa kwa mujibu wa
Jaji Warioba ni Muundo wa serikali
Tatu, umependekezwa kutokana na
sababu mbili.
1. Kwamba watanzania wengi
wamependekeza muundo huo
2. unatoa majibu ya matatizo ya
serikali mbili
Friday, 21 March 2014
Hotuba ya kipuuzi kabisa kuwahi kutolewa na kiongozi wa kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment