Talking hints za Katibu Mkuu kwenye press conference Oktoba 16, 2014.
Kamati Kuu ilikuwa na jumla ya agenda kumi na moja, mengine tutayatoa kwa umma kadri muda unavyokwenda.
Kwa leo tutazungumzia masuala mawili ambayo yana sura ya utekelezaji,
tena wa muhimu na haraka; Mchakato wa Katiba Mpya na Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa;
Katiba;
Tunawataka Watanzania wanaopenda nchi yao sasa waache kulia lia, waache
kunung’unika pekee, waache kulalamika. Tuingie kazini. Sasa ni wakati wa
kuingia kazini.
Wenzetu tangu siku ya kupokea rasimu ambapo Kikwete si kama rais wa
nchi, bali kama Mwenyekiti wa CCM alianza kuipigia chapuo debe Katiba
Inayopendekezwa. Sasa tuingie kazini…
Kikwete kama mwenyekiti wa CCM akitumia kofia ya rais wa nchi, baada ya
kupokea rasimu ameendelea kuipigia chapuo, anawaambia wananchi wasome
Katiba inayopendekezwa waelewe, sisi tunamwambia aache kuwadanganya
Watanzania. Katiba si sawa na novel kwamba kila mtu anaweza kuisoma tu
na kuelewa, ingelikuwa ni rahisi namna hiyo tusingekuwa na haja ya
kuwasomesha akina Lissu (Tundu).
Tunahitaji wananchi wetu wasaidiwe tafsiri hasa ya katiba yenyewe na
maana yake, hadi yale mambo ya ndani kabisa. Ndiyo kazi ambayo CHADEMA
tunaanza kuanzia kesho kuzunguka nchi nzima, ambapo timu ya kwanza
itaongozwa na BAWACHA. Ujumbe utakuwa ni Katiba Mpya na Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa. Tunataka kuwafafanulia Watanzania kwa kina.
Wakati bado tunapigania Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Uchaguzi
Mkuu wa mwaka kesho, moja ya ujumbe wetu kuanzia sasa ni kuwataka
Watanzania kujiandaa kufurika vituoni kujiandikisha kwenye daftari la
wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambalo litaanza
kuandikishwa siku 21 kabla ya uchaguzi wenyewe.
Watanzania wafurike kwa wingi. Wajiandikishe. Kuiondoa CCM kunahitaji vitendo. Tuingie kazini.
Kwa mtindo huo huo wa kuingia kazini sasa kwa vitendo, tutatembea nchi
nzima sasa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi sana siku ya Desemba
14, kupiga kura kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na
Vitongoji…
Tunawaagiza vile vile viongozi wetu katika ngazi zote za chama, kuanzia
kanda, mikoa, wilaya, majimbo, kata, matawi na hadi misingi kuwaongoza
Watanzania wote; 1. Kujiandikisha, 2. Kupiga kura na 3. Kusimamia
taratibu za kikanuni…
Tumeshabaini na kila Mtanzania sasa anajua kuwa kuwa Rais Kikwete si mtu
wa kuaminika tena…ni mtu anayebadilika badilika na wala haoni haja ya
kuomba samahani…
Na sasa tumezidi kubaini kuwa Kikwete amefikia mahali pa kugeuka kuwa
procurement officer na tumenasa nyaraka ambazo zinaonesha kuwa katika
kujigeuza ofisa manunuzi huko yanafanyika maandalizi ya kufanya
mapambano na wananchi badala ya kuandaa maridhiano.
Nyaraka…Rais amegeuka kuwa Ofisa Manunuzi, Ofisa Mawasiliano TCRA
Tumepata taarifa za ziara yake ya kwenda China. Siwezi kusema atakwenda
tarehe ngapi maana mimi si kazi yangu kutangaza tarehe za ziara za
Kikwete ambazo sasa hata tumechoka kuhesabu maana zimeshakuwa nyingi mno
zaidi ya 300+ ndani ya miaka kumi.
Kilichotushtua si Kikwete kwenda ziara, maana siku hizi wala si habari
tena, kilichotushtua ni hicho kinachompeleka huko China…ukimsikiliza
Kikwete kwenye mazungumzo anapenda kuonekana mtu anayeoenda amani,
mshikamano lakini si kweli.
Amejigeuza Ofisa Manunuzi. Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na jitihada za
kupata helkopta tatu mpya…zingelikuwa ni kwa ajili ya Jeshi letu la
Wananchi nisingekuwa na shida, shida inakuja namna zinavyotafutwa.
Zinatafutwa kwa utaratibu ule ule wa kifisadi uliotumika kununua ndege
ya rais wakati ule na hata rada.
Tena anamtumia kampuni moja hivi ambayo tumekuwa tukiituhumu katika
ufisadi. Sasa sisi tunahoji, hivi ni kwa nini Serikali ya CCM inashindwa
kwenda kiwandani na kufanya order ya manunuzi kiwandani moja kwa moja
hadi itumie taratibu za kifisadi au mafisadi kufanya kazi hizi…
Kikwete anajua kuwa ninajua. Maana ameshalalamika kwa watu wake wa
vyombo vya dola kwamba taarifa hizi zimefikaje kwa Dokta Slaa…
Wametumia fedha zetu za mikopo kutoka Ujerumani…ndege zinanunuliwa
Ufaransa…anatuma fisadi kwenda kufanya manunuzi hayo badala ya Serikali…
Kinachoonekana na taarifa na sisi hapa tunahoji je ni kweli ndege hizo zinataka kutumika kwa manufaa ya CCM?
Rais pia ameomba kwenda Beijing kufuatilia mitambo ya Police
Surveillance System…wanataka mitambo hiyo ifike hapa kabla ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015…ujumbe huu umeandikwa na mtu anaitwa Mbelwa…Kairuki.
Waandishi wa habari mtakuwa mnajua huko Wizara ya Mambo ya Nje.
Anamwandikia Waziri wa Mambo ya Nje…ujumbe huu umeandikwa tarehe
7/10/2014…
Sasa hizo ndege anayotaka kununua iko mji mwingine huko China si ule
aliopangiwa katika ziara yake, sasa imeagizwa irushwe hadi pale
atakapokuwa ili eti Rais mwenyewe aweze kuiona…nimeangalia kwenye budget
component hiyo kitu hakuna. Kwa kawaida vitu vya kijeshi huwa havitajwi
kwenye bajeti, lakini kwenye randamana ungeweza kuona mpango wa kununua
kitu kama hicho. Hakuna.
Sasa kinachoonekana ni kwamba kwa sababu wamejua mwaka 2015 wanaondoka
madarakani, wanaanza kujiandaa kwa mapambano badala ya maridhiano.
Nataka kumwambia Rais Kikwete kwamba nchi haiongozwi kwa misuli,
haiongozwi kwa kutunishiana misuli. Wanataka kufanya kama walivyofanya
majuzi kutunga Katiba Mpya kwa mitutu ya bunduki.
Sasa tena uchaguzi unakaribia wanaanza maandalizi ya mitutu…tunamwambia
Kikwete sisi tutakuwa wa mwisho kuona nchi hii inaingia katika vurugu.
Ndiyo maana ili kuepusha mambo mabaya yasitokee kila taarifa kama hii
tukiipata tutapiga kelele. Silaha kubwa ya mnyonge ni kupiga kelele.
Katika mwendo huo huo wa Rais Kikwete kugeuka kuwa Ofisa Manunuzi, sasa
amejigeuza kuwa Bwana TCRA, wanapanga kukutana na Kampuni ya HUAWEI ya
China ili wanunue mtambo utakaowekwa ikulu kwa ajili ya kunasa simu za
akina Dokta Slaa…
Mitambo hiyo inapelekwa ikulu badala ya…ingepelekwa Usalama wa Taifa
ningeelewa, ingepelekwa kwenye Jeshi letu ningeelewa, lakini ikulu?
Tunasisitiza hatuna tatizo kama mambo haya ya ndege, helkopta au mitambo
ya mawasiliano yangekuwa yanafanywa kwa ajili ya ulinzi na usalama wa
nchi, lakini ni tatizo kubwa kama rais ndiye anakuwa Ofisa wa Manunuzi
au Ofisa wa Mawasiliano, TCRA.
Sasa wanatafuta na kuhangaika kutafuta kila njia ya kubaki madarakani.
Tunamuonya Rais Kikwete kuwa hizo pesa anazotaka kuchezea kwa yeye kuwa
Ofisa Manunuzi si za mfukoni mwake. Aache kuchezea fedha za Watanzania.
Tulimuonya pia hivi hivi wakati alipochezea fedha za Stimulus Package.
Kama anataka kutukamata atukamate lakini sisi tutasema. Haya ndiyo mambo
ya madhara ya katiba inayopendekezwa, kama ambavyo tumeshasema vizuri
mapema.
No comments:
Post a Comment