Monday, 15 September 2014

DIWANI ALLY NKANGA WA CCM AJIUNGA NA CHADEMA

Diwani Ally Nkanga wa Singida Magharibi na Makamu mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Ikungi Singida Magharibi amejiunga na chadema, na kukabidhiwa kadi ya Chadema kwenye mkutano wa baraza kuu la chadema linalofanya mkutano wake Mlimani City Dar Es Salaam. Chadema inaendelea kubomoa ngome za CCM. Diwani huyo akizungumza mbele ya baraza kuu, ameeleza kwamba CCM siyo sehemu salama tena, badala ya kuwatumikia watanzania, wamewageuza watanzania kama kitega uchumi. Amesema chama pekee ambacho kimeonyesha nia na dhamira njema, yenye kukidhi matarajio na matamanio ya watanzania ni CHADEMA, na yeye kwa dhati kabisa, bila kushawishiwa na mtu yeyote ameamua kuungana na timu ya ukombozi.

No comments:

Post a Comment