Sunday, 20 July 2014

MKUTANO WA CHADEMA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAAZIMIO YA KAMATI KUU 20/7/2014

Mwenyekiti Freeman Mbowe anasoma maazimio ya Kamati kuu kuwa kamati kuu imeazimia yafuatayo

CHADEMA kama sehemu ya UKAWA itaendeleza mazungumzo ya kunusuru mchakato wa Katiba

Pia kamati kuu imewaagiza wabunge wake ambao ni sehemu ya UKAWA kurejea Bungeni ikiwa tu Mamlaka ya Bunge la Katiba itafafanuliwa juu ya kutobadili misingi mikuu ya Rasimu ya Katiba

Kamati Kuu imekiagiza chama ikiwa hakutakua na mabadiliko katika mtazamo wa chama tawala kuhusu mamlaka ya bunge la katiba basi chama kisusie mchakato huu na endapo kama bunge la katiba litaendelea basi CHADEMA kijiandae kama sehemu ya UKAWA kuhamasisha wananchi nchi nzima kuipinga Rasimu itakayotolewa

Uchaguzi Serikali za Mitaa:

Mwenyekiti amesema kuna hila nyingi na kauli za kutofautiana zinazotolewa na viongozi wa Serikali.

Amesema waziri mkuu Mizengo Pinda amekuwa akitoa kauli za kujichanganya kila anapozungumzia uchaguzi huu.Mbowe amesema lengo kubwa la Serikali ni kuhujumu upinzani katika uchaguzi huu muhimu.

Mwenyekiti amesema Kamati kuu inatamka wazi Chadema ina nguvu kote nchini na imejiandaa vya kutosha na hata kama uchaguzi huu ukifanyika KESHO Chadema itashiriki na CCM itarajie aibu kubwa kwa sababu Watanzania wamewakataa.

Kuhusu hali ya Kisiasa ndani ya Chama

Kamati kuu inawataka wananchi,wanachama na wapenzi kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mapambano makali dhidi ya chama chetu.

Wasaliti wa sasa na wa Baadae hawataweza kamwe kufifisha nguvu ya mapambano haya tunapojiandaa na uchaguzi mkuu Mwakani

Taarifa za kuhama kwa baadhi ya viongozi wa kanda ya Magharibi hazitarudisha nyuma nguvu za Mabadiliko.

Si mara ya kwanza kwa chama tawala kutumia mawakala wao katika mazingira haya ambayo CCM ipo katika hali mbaya ni lazima wangefanya hivyo.

Tutakilinda chama hiki kwa gharama zozote zile.Hiki sio chama cha kufuga wasaliti.Unapoona chama cha upinzani kinafadhiliwa na chama cha mapinduzi kupambana na chama cha upinzani mjiulize maswali .

Harakati za mapambano hazitarudi nyuma tumejipanga vyema kuliko wakati mwingine wowote.

Tunajiandaa na uchaguzi ndani ya chama.Kuna watu waliona kwamba hawataweza kuhimili uchaguzi kutokana na udhaifu na historia yao ya usaliti .

Hatukupenda kuwafukuza badala yake tuliwaacha wajitathmini waone kama wanatosha.

Uongozi uliondoka Kigoma umekuwepo madarakani tangu mwaka 1993.Wamejiona hawatoshi,tunawashukuru kwa kusoma alama za nyakati.Tunawatakia kila la Kheri.

Chama kina Network Kubwa sana ambayo haijawahi kufikiwa na chama hiki tangu kimeanzishwa.

Tunasonga mbele kwa mapambano haya na kwa Uhakika tutashinda.

Asante sana wanahabari."

Maswali kutoka kwa Wanahabari:

Mwenyekiti anajibu maswali ya waandishi wa Habari.

Anasema kama kuna mtu anadhani anaweza kukiyumbisha chama hiki kwa fedha ajitafakari upya.Viongozi wakuu wa chama hiki hawatayumbishwa kwa vitisho au fedha.

Tunaongoza mapambano .Kama kuna watu wanaotaka kusaliti mapambano haya kwa tamaa ya fedha watoke haraka sana .

Mwisho:

Mwenyekiti anawashukuru tena wanahabari ambao wamefurika mpaka wengine kukosa sehemu ya kukaa.

Anasimama na kuondoka na viongozi wake wakuu Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa Makamu Mwenyekiti Said Issa Mohamed,wakurugenzi wote wa makao makuu na wajumbe wote wa Kamati Kuu.

No comments:

Post a Comment