Saturday, 19 April 2014

Ikulu Iombe Radhi

By Ben Saanane,

Namnukuu Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM Taifa 'Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu kumtukana na kuwakejeli waasisi" Kisha naendelea kunukuu " "Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo aliijenga yeye ndiyo imeendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka pate hii. Viongozi wengine wale ambao wamemfuata yeye — Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa mimi mwenyewe, tumefuata na kuongozwa na misingi hii. Na siku nchi yet inaamua kuipuuza misingi hiyo, tutaingia katika matatizo makubwa." -Rais Jakaya Kikwete akinukuliwa kupitia Taarifa ya Mawasiliano Ikulu.

Naomba kuhoji .Ni nani anayemtukana na kumkejeli Baba wa Taifa hapa

Unafiki pembeni sasa.Je misingi ya kuzika azimio la Arusha ndiyo inayojenga heshima kwa Nyerere?

Je Nyerere anaheshimika kwa Rais Mkapa Kuruhusu uuzaji wa Benki ya NBC tena benki ya Umma kwa Shilingi milioni chache tu (Bei ya kutupwa)kwa mabepari wa Kikaburu?

Je,Nyerere anaheshimika na kuenziwa kwa Mkapa kujimilikisha Mradi wa Kiwira (Tuma ambazo hajawahi kukana)?

Je,Nyerere anaenziwa kwa Rais Mkapa kuongoza nchi ambayo Zaidi ya Bilioni 100 na ushehe kuchotwa Benki Kuu bila yeye kujua?

Je,ni heshima kwa Nyerere na misingi yake kuruhusu wezi wa EPA kurudisha fedha bila hatua za kisheria ?Kwamba Nyerere aliwahi kujivunia kufanya majadiliano na wezi na mafisadi wa mali za umma?

Je,Nyerere hatukanwi kwa kuruhusu Dhahabu kuchimbwa kwa misamaha holela bila kulipa kodi huku wananchi hasa Geita wakigeuzwa kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao bila vita?

Je,Misingi ya Nyerere ndio iliyoruhusu vijana kugeuzwa manamba kwenye makampuni ya madini huku wakifa vifo vya kikatili kutokana na mazingira hatarishi ya kufanya kazi?

Hivi tamko hili sio kejeli kwa baba wa Taifa na misingi yake?

Ujamaa na kujitegemea ndio msingi wa Taifa letu.Je Taifa letu na hata chama tawala alichokiasiasi Mwl.Nyerere kinafuata misingi hiyo?

Je,CCM ni chama kinachotetea maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi wanaokatwa kodi Asilimia 18 na Zaidi ya mishahara kiduchu huku mabepari waliowekeza kwenye Migodi yetu wakipata misamaha ya kodi na wengine kuwezeshwa kukwepa kodi?

Ni nani anayemkejeli Mwalimu Nyerere hapa?

Washauri wa Rais Ikulu walitakiwa kumshauri Rais kabla ya kutoa Tamko ambalo litaamsha hasira na hisia za uchungu miongoni mwa jamii ya Watanzania

No comments:

Post a Comment