DCI AMUUMBUA RC ARUSHA
Katika hatua nyingine DCI, Mngulu
alikanusha taarifa zilizowahi kutolewa na
mkuu wa Mkoa, Mulongo mwezi agosti
mwaka jana kuwa polisi wamefanikiwa
kukamata wahusika wa mtandao wa
walioingiza mabomu ya kurushwa kwa
mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph
Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na
kwenyemkutano wa wa hadhara wa
Chadema, Soweto mkoani Arusha.
DCI aliendelea kusisitiza kuwa wao kama
watendaji wa jeshi la polisi mpaka sasa
hawamshikilii yeyote kuhusiana na tukio
la Soweto zaidi ya mtu mmoja
aliyefikishwa mahakama kuhusiana na
tukio la bomu la kanisani.
" Msichanganye masuala ya utendaji na
siasa, sisi Jeshi la polisi hatujakama mtu
hayo nayodai mmelezwa na mkuu wa
mkoa nendeni mkahojiane naye awaeleze
hao anaodai kuwa wanahojiwa mbona
hawajafikishwa mahakamani, nimesema
muulizeni yeye (RC) ,huyo ni msemaji wa
serikali, hayo aliyowaambia mrudieni
mkamuulize yeye, sisi kama polisi hatuna
taarifa kama hiyo''alisema Mngulu.
Vyombo mbalimbali vya habari
vilimnukuu Mulongo wakati wa mkutano
wa siku moja wa kuzungumzia fursa za
uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika
eneo la Olasiti akidai kuwa Polisi wako
katika hatua za mwisho za mahojiano na
watuhumiwa hao, ambapo mbali na
kutaka kufahamu waliowatuma na
malengo yao, pia wanatarajia kupata
taarifa za waliorusha mabomu hayo.
"Watuhumiwa hawa siku si nyingi
Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka
majina hadharani, watu wawajue na si
wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa
ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza
mabomu hayo na kwa lengo gani,"
alinukuliwa mkuu huyo wa mkoa.
Hata hivyo Mulongo alipopigiwa simu na
mwandishi wa habari hizo na kuulizwa juu
ya jambo hilo alisikiliza kisha akakata
simu bila kutoa majibu ambapo
alipopigiwa tena simu hiyo ilikuwa
imezimwa kabisa.
Sunday, 20 April 2014
DCI AMUUMBUA RC ARUSHA
Na Grace Macha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment