Ukweli ni kwamba pamoja na CCM kumsimamisha mtoto wa Marehemu Mgimwa bw. Godfrey Mgimwa, hakuweza kujenga ushawishi wa kuvutia hisia za wananchi wa Kalenga kama ambavyo amefanya mgombea wa CHADEMA kamanda Grace Tendega. Tendega na CHADEMA walifanikiwa sana kuendesha kampeni za kisayansi hadi dakika ya mwisho, lakini cha kustaajabisha sana matokeo yamekuja tofauti na matarajio ya kila aliyekuwa ameshuhudia mikutano ya kampeni.
Maswali ambayo watu wengi wanauliza ni;
je, CCM waliiba kura?
je, Mawakala wa CHADEMA walifika bei?a
je, Watu waliokuwa wanahudhuria mikutano hawakujiandikisha?
Juu ya maswali hayo hapo juu ninaamini CHADEMA kama chama makini kitafanya uchunguzi wa kina na kubaini mapungufu yaliyojitokeza, maana waswahili husema "Wali wa kushiba unauona kwenye sahani", lakini hili limekuwa kinyume chake.
ukweli utabaki kuwa ccm inacheza na umaskini na ujinga wa watanzania, mfano hakukuwa na sababu ya watu wa kalenga kuipa kura ccm. CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo wana Kalenga, hakuna zahanati, hakuna walimu, hakuna maji, hakuna barabara kwa miaka yote zaidi ya 50 ya uhuru wa nchi hii.
Hata hivyo kama sitakosea, kwa wale wenzangu na mimi tulioshuhudia trend ya wapiga kura, tunaweza kuona tofauti ya watu waliopiga kura na watu waliokuwa wanahudhuria mikutano ya CHADEMA na CCM ni tofauti kabisa.
nimeshuhudia haya yafuatayo;
- Asilimia zaidi ya 85 ya waliopiga kura ni wazee ambao siyo wahudhuriaji wa mikutano ya kampeni.
- Wapiga kura karibu waliokuwa kwenye foleni ya kupiga kura walikuwa wamelewa chakari, hii inaonyesha kabla ya kupiga kura walikuwa wanapitia mahali wananyweshwa pombe ndiyo wanaambiwa wakapige kura. Hili linatia mashaka kama wapiga kura walifanya uchaguzi sahihi, ama walipiga kura kulipa fadhila ya aliyewalewesha. Niliwahi kuambiwa watu wa Iringa hasa wahehe huwa wana roho ya huruma kwa mtu aliyewasaidia chochote kile mfano kuwanunulia pombe, soda, t-shirt, kofia ama khanga.
Pamoja na CHADEMA kukaa chini na kufanya tathmini, baada ya kurudi kwenye field agenda ya kwanza na ya msingi kuliko zote iwe UBORESHWAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA. Kutokuboresha la wapiga kura kunawafanya CCM waendelee kutamba na wazee ambao siyo sehemu ya mabadiliko tunayoyataka, kwa maana ya kwamba wengi wao siyo wasomi na ni wachache wanaofanya utafiti na kushiriki katika siasa. Tume huru ya Uchaguzi iwe jambo la pili. Kuna watanzania zaidi ya 60%
Kushindwa kwa Kalenga sasa iwarudishe mezani watafakari kwani kila chaguzi ccm wanashinda? Mfano kati ya kata 27 CHADEMA walifanikiwa kushinda kata 3 tu. Kalenga CCM wameshinda kwa zaidi ya 79%.
No comments:
Post a Comment