Sunday, 16 March 2014

PROGRAMU YA UDHAHILI WA WANACHAMA WA CHADEMA IMEFANIKIWA KWA 90% Arusha na Manyara

Kama tunavyokumbuka chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kilianzisha programu ya kudhahili wananchama wake nchi nzima, yaani program ya CHADEMA NI MSINGI ili kukasimisha madaraka kuanzia ngazi za misingi hadi taifa.

Hii program kwa upande wa Arusha kwa ujumla imefanikiwa kwa zaidi ya 90%, kwa mfano katika kata zote 19 za wilaya ya Arusha mjini takriban kata 18 tayari zimeshafanya uchaguzi wa ngazi za misingi, na zingine uchaguzi wa matawi tayari zimefanyika.
Mfano mwingine kata ninayotoka nimeshuhudia chaguzi za misingi ikiendelea katika kata ya Olasiti, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chadema ni msingi kata ya Olasiti kamanda Oscar Lyatuu, uchaguzi wa matawi yote kata uwe umefanyika kabla ya mwisho wa mwezi wa March 2014, kwa maana hiyo tayari chaguzi za misingi inafikia ukingoni kwenye kata yake ya olasiti.
Mratibu wa Chadema ni Msingi jimbo la Arusha mjini kamanda Frances Steven naye amethibitisha kuwa kata ambayo bado uchaguzi wake haujafanyika ni kata ya Terat, ambayo kwa wiki mbili zijazo utakuwa tayari.

Jambo la kutia moyo kwenye zoezi la kudhahili wanachama wa chadema ni msingi kwa upande wa manyara hasa babati vijijini imefanikiwa pengine nisema kwa 100% maana imesomba achilia mbali mabalozi wa nyumba kumi, lakini pia viongozi wa serikali za mitaa pia. Pongezi nyingi zimemwendee Laurent Tara na Paulina Gekul.

Kimsingi lengo la hii program imeandaliwa mahususi na chama makao makuu kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao 2015. Uchaguzi wa chadema ni msingi kila mahali unaenda sambamba na usimikaji wa mabalozi wa nyumba kumi.

No comments:

Post a Comment