Tukio la utekaji na utesaji limechukua sura mpya, baada ya polisi kuamua kushirikiana na green guards wa ccm kuteka mawakala wa chadema waliokwenda kusimamia uchaguzi Kalenga.
Tukio hili lina mtiririko kama nitakavyoelezea hapa chini.
Jana Polisi wakishirikiana na RCO wa Iringa walilikamata
gari T808AMX ambalo ndani yake kulikuwa na watu wanne akiwemo Kamanda Walter
Munuo pamoja na katibu wa mbunge suzan lyimo kamanda Edward, walikamatiwa kata
ya Ifunda, wakawapeleka kituo cha polisi Ifunda, baadaye wakakubaliana
kuwapeleka kituo kikuu cha polisi Iringa. Baada ya kukamatwa RCO alitangaza
kupitia local media kwamba wameikamata gari la CHADEMA lenye namba T 808 AMX
likiwa limebeba mawe na visu ndani.
CHADEMA walipofuatilia kituo cha Polisi kujua hali ya watu
wao, polisi wakakana kulikamata gari hilo, na watu hao. Hivi tunavyozungumza
hao watu pamoja na gali hawajulikani walipo. Hata hivyo taarifa za awali
zinasema baada ya kutoka kituo cha polisi cha Ifunda, RCO na vijana wake
waliwapeleka wale vijana pamoja na gari tajwa ofisi ya ccm Iringa,
wakawakabidhi kwa Green Guards. CHADEMA wanafanya kila jitihada kujua wenzetu
wamepelekwa wapi na wamefanywa nini.
Jana hiyo hiyo tukio linguine lilikuwa la kukamatwa kwa
kamanda Derick Magoma, ambaye polisi kwa kudhihirisha kuwa wao ni makada wa ccm
walimbambikizia wakala wetu Magoma kesi ya kumiliki silaha aina ya SMG, jambo
ambalo ni uwongo na uzandiki wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa. Magoma bado
anashikiliwa kituo cha polisi Iringa.
Tukio linguine mawakala Danstun na wenzake jana walitekwa na green guards/magaidi wa ccm,
walitekwa na magaidi wenye toyota surf nyeusi ikiongozwa na mtu moja
anaitwa Mollel, Emma na wenzake watano majira ya saa sita wakiwa eneo la
darajani, wakapigwa na kudhalilishwa sana pale pale wakiwa pamoja na
binti watatu hivi, wakapelekwa ofisi ya ccm mkoa wa Iringa badala ya
kuwapeleka polisi, Godfrey Mgimwa na mabaunsa wake wakafika pale,
waliwashambulia sana mbele ya Mgimwa wakawapiga sana wakasema hawa
waliingia Iringa na hawatatoka Iringa mtu wa kwanza kufika pale alikuwa
Hassan Mpenga katibu wa CCM mkoa wa Iringa, wakawa wanafanya mazungumzo
halafu wanaendelea kutupiga tu. Walituvua nguo wakawa wanatupiga
picha.
Ilipofika saa tatu hivi wakati ccm wanashangilia ushindi tukapakiwa kwenye cruiser nyeupe, tukapelekwa msitu wa nduli, tulipofika katikati ya msitu walituamrisha tulale chini ya gari. Wakatupakia tena kwenye gari, wakatuamrisha tutoke moja moja, wakamtoa mwenzangu moja anatokea morogoro akawa wa kwanza kushushwa wakaingia naye kwenye chaka, cha kushangaza wale jamaa walikuwa na dumu la petroli, sring ndefu, panga na kudu (kamba) na bastola mbili. kwa dakika zile zile kukawa kuna canter moja ilikuwa inapita, gaidi moja aliyekuwa ameachwa kwenye point ya barabara akawa anakimbilia gari na kumwambia dereva aliyekuwa anamchunga na kumwambia awashe gari haraka litembee, ili isionekane gari limepaki, ikawa ndiyo bahati yake wakati gari linatembea yeye aliruka kwenye gari na kuanza kukimbilia ile canter.
Wakawa wanamkimbiza Danstun, alipoona wale jamaa wanamkimbiza na wana silaha aliingia vichakani, wakamtafuta kwa kipindi kifupi wakaanza kubishana, wakaanza kumlaumu dereva amefanya vitu vya ajabu sana, wakawasha gari wakaondoka, akakaa kwa muda wa kama lisaa limoja hivi, akaanza kutembea usiku mpaka saa nane hivi akawa amefika mji mwema, akafika kwenye nyumba moja akafanikiwa kupata simu ili akawasiliane na Kigaila. Kweli dereva wa yule gari alisikitika sana machozi yanamtoka akasema hakuna jinsi lazima atakufa, na moja wa wauwaji wale ni askari wa usalama wa taifa. Amelalamika kuwa wauwaji hawa inawezekana wanatekeleza agizo la mkuu wa nchi.

Mpaka hivi sasa haijulikani yule kijana aliyeshushwa porini
haijulikani alipo, haijulikani amefanywa nini.
No comments:
Post a Comment