Tuesday, 18 March 2014

KAULI YA JK YATIMIA KALENGA


CHADEMA wasimulia walivyoteswa kwenye Msitu wa Nduli


http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/03/kalenga5.jpg

KAULI ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete kutaka wanachama wa chama hicho kuacha upole na kujibu mapigo kwa wapinzani imetimia katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.
Kauli hiyo inaelezwa kutimia jimboni Kalenga baada ya wafuasi wa CCM kudaiwa kuwafanyia vitendo vya kinyama wafuasi na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa kampeni hadi siku ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga.
Matendo hayo ya kinyama ni pamoja na kupigwa, kutekwa, kuteswa na hata kubakwa ambako kunadaiwa kufanywa na walinzi wa CCM, maarufu kwa jina la Green Guards.

Hatua ya Green Guards kuteka na kutesa ilifikia pia kutekwa kwa Mbunge wa viti maalum CHADEMA Rose Kamili, ambaye alipigwa sana, akateswa sana na kunyang'anywa pochi na simu zake zote pamoja na fedha. Rose alilazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa, na baadaye kuhamishwa hospitali ya rufaa ya KCMC.

No comments:

Post a Comment